Mpango Shirikishi wa Usimamizi wa Msitu wa Cheptongei (2024-2029)

Mifano ya kurasa zilizotumiwa

Muhtasari

Mpango Shirikishi wa Usimamizi wa Misitu wa Cheptongei unaeleza mbinu ya ushirikiano ya usimamiaji endelevu wa hekari 23,350.7 za Msitu wa Cheptongei, unaojumuisha sehemu maeneo ya Kapchemutwa, Sogotio, Cheboyit, na  Kipkunur. Ulichapishwa katika Gazeti rasmi kati ya mwaka wa 1941 na 1967, msitu huo unasimamiwa na Huduma ya Misitu ya Kenya (KFS) kupitia Kituo cha Misitu cha Cheptongei. Mpango huu uliundwa kwa kuhusisha kwa kiwango kikubwa washikadau, pamoja na jamii za wenyeji kupitia Shirika la Misitu la Jamii la  Cheptongei, mashirika ya serikali kama vile KWS, NEMA, WRA, na Serikali ya Kaunti ya Elgeyo Marakwet, na kufadhiliwa na Hazina ya Maji ya Eldoret Iten. Mpango huo unalenga kusawazisha uhifadhi na maendeleo ya jamii, ukitumia mfumo jumuishi unaounga mkono uhifadhi wa misitu na maisha ya wenyeji. Maono yake ni kuendeleza Cheptongei kama msitu uliohifadhiwa vizuri unaotekeleza jukumu muhimu katika ngome ya maji ya Cherangany na zaidi.

Mchango wetu

Kuhariri
Uhariri wa kina
Kusahihisha

Usanifu
Usanifu wa michoro
Uchapishaji kupitia tarakilishi

 Uchapishaji
PDF Iliyo tayari kuchapishwa
Faili ndogo ya PDF iliyo rahisi kushiriki na watu mtandaoni

 Mwaka wa uchapishaji: 2025

Lengo la Malengo ya Maendeleo Endelevu linalohusiana na chapisho