Mpango Shirikishi wa Usimamizi wa Msitu wa Cherangany
Mifano ya kurasa zilizotumiwa
Muhtasari
Mpango Shirikishi wa Usimamizi wa Msitu wa Cherangany (PFMP) ni mkakati wa miaka mitano unaolenga kuweko kwa usimamizi na uhifadhi endelevu wa hekari za Msitu wa Cherangany katika Kaunti ya Elgeyo Marakwet, nchini Kenya. Ulichapishwa katika Gazeti rasmi mwaka wa 1964, msitu huo unajumuisha Chemurgoi, Koisungur, Kipteber, na Kerer, na unasimamiwa na Huduma ya Misitu ya Kenya (KFS).
Mpango huo uliundwa kupitia mashauriano yaliyojumuisha jamii za wenyeji, mashirika ya serikali, na mamlaka ya mazingira, na kufadhiliwa na Hazina ya Maji ya Eldoret Iten, mpango huo unasisitiza mbinu ya ushirikiano katika uhifadhi. Unakusudia kutengeneza upya maeneo yaliyoharibika, kulinda vyanzo vya maji, kuhamasisha uhifadhi wa wanyamapori, na kuboresha maisha ya watu kupitia kilimo cha misitu na utumiaji endelevu wa misitu. Zaidi ya hayo, kwa kuelekezwa na maono ya pamoja ya kuwa kiongozi katika usimamizi endelevu wa misitu, PFMP inashirikiana na Sheria ya Uhifadhi na Usimamizi wa Misitu ya Mwaka wa 2016. Mikakati muhimu iliyopendekezwa katika mpango huo ni pamoja na upandaji wa kusitawisha, elimu ya misitu, usimamizi wa mashamba ya mitiulioboreshwa, na udhibiti wa matumizi ya maji—ukihakikisha kwamba Msitu wa Cherangany unaendelea kusaidia viumbe mbalimbali na usitawi wa jamii kwa ajili ya vizazi vingi vijavyo.
Mchango wetu
Kuhariri
Uhariri wa kina
Kusahihisha
Usanifu
Usanifu wa michoro
Uchapishaji kupitia tarakilishi
Uchapishaji
PDF Iliyo tayari kuchapishwa
Faili ndogo ya PDF iliyo rahisi kushiriki na watu mtandaoni
Mwaka wa uchapishaji: 2025




