Ni Ulimwengu wa MICE

Mifano ya kurasa zilizotumiwa

Muhtasari

Kampuni ya Zuri Events ilizindua tena gazeti lake linaloitwa  Ni Ulimwengu wa MICE katika kongamano lake lililofanyika tarehe   9–11 Septemba 2025 katika Jumba la  KICC, Nairobi, ikiashiria tukio lake la kwanza la mkutano wa ana kwa ana tangu kuwepo kwa janga la COVID-19 na sherehe ya kumbukumbu ya  18 ya kampuni. Gazeti hili limerudi tena likiwa na mwelekeo mpya, na sasa linachapishwa kila robo ya mwaka (matoleo matatu kwa mwaka).

Kusudi la gazeti la Ni Ulimwengu wa MICE lilikuwa ni kuelekeza uongozi wa kimawazo katika nafasi ya Mikutano, Motisha, Makongamano na Matukio, katika kiingereza herufi  za kwanza ni (MICE), ili kuimarisha mahusiano, kujenga ushirikiano mpya, na kuangazia hadithi za mafanikio katika sekta mbalimbali. Hadhira yake inajumuisha Serikali, Mashirika ya Serikali za Kimataifa, Mashirika ya Kimataifa Yasiyo ya Serikali, watunga sheria, na sekta ya kibinafsi.

Katika mazingira yanayobadilika baada ya janga hilo, ambapo mienendo ya ufadhili na mahitaji ya sekta yamebadilika, gazeti hili linajitambulisha kama lenye mamlaka katika kuelezea jinsi sekta ya MICE inavyokua na kujiendesha kulingana na hali hizi mpya.

Mchango wetu

Kuhariri
Uhariri wa kina
Kusahihisha

Usanifu
Usanifu wa michoro
Michoro na usanifu wa vielelezo vya taarifa
Usanifu wa Tangazo
Uchapishaji kupitia tarakilishi

 Uchapishaji
PDF Iliyo tayari kuchapishwa
Faili ndogo ya PDF iliyo rahisi kushiriki na watu mtandaoni

Mwaka wa uchapishaji: 2025

Lengo la Malengo ya Maendeleo Endelevu linalohusiana na chapisho