Maono ya Karne ya Mwaka wa 2060: Kuijenga Somalia yenye amani, mafanikio, na ya kujivunia kufikia mwaka wa 2060

Maono ya Karne ya Mwaka wa 2060: Kuijenga Somalia yenye amani, mafanikio, na ya kujivunia kufikia mwaka wa 2060

Muhtasari

Maono ya Karne ya Mwaka wa 2060 (CV2060) ni mpango wa kijasiri wa taifa la Somalia kuwa nchi ya mapato ya juu ya kiwango cha kati yenye amani, mafanikio, na ya kujivunia kufikia mwaka wa 2060—karne yake ya uhuru. Yakikita mizizi katika mashauriano ya nchi nzima na hali halisi za Somalia, Maono hayo yanakuza umoja, suluhisho zinazotoka nchini, na maslahi ya taifa. Taarifa hiyo inaeleza njia za mabadiliko ya utawala jumuishi, ukuaji imara wa kiuchumi, ushikamano wa kijamii, na uendelevu wa kimazingira. Yakiongozwa na Baraza la Kitaifa la Uchumi na kuungwa mkono na washirika wa nchini na wa kimataifa,  CV2060 inawakaribisha Wasomali wote—walio nchini na ng’ambo—wawe washika dau wenye vitendo. Kwa ushirikiano wa kujitolea na uongozi wenye maono, Somalia inalenga kuishinda hali yake ya zamani na kuunda siku za baadaye zenye furaha, na zilizo imara zaidi kwa vizazi vijavyo.

Mchango wetu

Kuhariri
Uhariri wa kina
Kusahihisha

Michoro na vielelezo vya taarifa
Usanifu wa michoro
Michoro na usanifu wa vielelezo vya taarifa
Uchapishaji kupitia tarakilishi

 Uchapishaji
PDF Iliyo tayari kuchapishwa
Faili ndogo ya PDF iliyo rahisi kushiriki na watu mtandaoni

Mwaka wa uchapishaji: 2025

Lengo la Malengo ya Maendeleo Endelevu linalohusiana na chapisho