Ushirikiano wa kimaeneo katika enzi ya migogoro mingi na ushindani wa mikakati ya kijiografia katika eneo la COMESA

Mifano ya kurasa zilizotumiwa

Muhtasari

Toleo la kitabu hiki linakusanya makala kutoka kwa kongamano la kwanza la kila mwaka la Chama cha Mahusiano ya Kimataifa cha Kenya (IRSK), lililofanyika Oktoba 2023 likiwa na maudhui haya Mahusiano ya Kimataifa na Diplomasia katika enzi ya migogoro mingi na ushindani wa kimkakati wa kijiografia katika eneo la COMESA.”

Kitabu hiki kinachunguza changamoto nyingi zinazolikumba eneo la COMESA, zinazojumisha na migogoro, mabadiliko ya tabianchi, misukosuko ya kiuchumi, upungufu katika utawala, na shinikizo za kijiografia na kimkakati kutoka nchi za nje, na athari zake kwa amani, usalama, na muungano wa kimaeneo. Kinasisitiza kwamba muungano si mradi wa kiuchumi pekee bali pia ni wa kisiasa na kijamii, unaohitaji taasisi zenye nguvu zaidi, utekelezaji bora wa sera, maono ya pamoja kati ya nchi za uanachama.

Likitumika kama rasilimali ya kielimu na pia kutoa wito wa kuchukua hatua, toleo hili la kitabu linawaalika watunga sera, watafiti, na washika dau wa kimaeneo kufikiri upya kuhusu mikakati ya ustahimilivu, ushirikiano, na maendeleo endelevu katika  COMESA.

Mchango wetu

Kuhariri
Uhariri wa kina
Kusahihisha

Usanifu
Usanifu wa michoro
Uchapishaji kupitia tarakilishi

Uchapishaji
PDF Iliyo tayari kuchapishwa
Faili ndogo ya PDF iliyo rahisi kushiriki na watu mtandaoni
Nakala zilizochapishwa

Mwaka wa uchapishaji: 2025

Lengo la Malengo ya Maendeleo Endelevu linalohusiana na chapisho